Kiwanda cha shayiri cha Kilimanjaro Malting Plant kilichopo mkoani Kilimanjaro kinatarajiwa kuanza kazi ifikapo mwezi Machi 2024.
Hatua ya kuanza kazi kwa kiwanda hicho inatokana na kukamilika kwa makubaliano ya kimkataba kati ya kiwanda cha Kilimanjaro na TBL makubaliano ambayo yatapunguza uagizaji wa zao la shayiri kutoka nje.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameeleza hayo katika mkutano uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Kilimo, ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya TBL, Jose Moran, Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Kamati ya Kudumu ya Bajeti pamoja na Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za Wizara ya Kilimo jijini Dodoma.
Amesema hatua itawanufaisha wakulima wa shayiri nchini kwa kupata soko la uhakika.
Mpango huo unakwenda kusaidia uzalishaji wa zao hilo katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Manyara na Kilimanjaro kutoka tani 5,000 hadi tani 12,000 na baadae kufika tani 32,000 baada ya miaka mitano kitakapokamilika.