• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Saturday, June 25, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

WAZIRI ATAKA UWEKEZAJI WENYE MANUFAA KATIKA JAMII

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Nchini Mhe. Angellah Kairuki

Jensen Kato by Jensen Kato
June 29, 2020
in UWEKEZAJI
0
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Nchini Mhe. Angellah Kairuki amewataka wawekezaji wote nchini kujihusisha na jamii zinazowazunguka kwa kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuleta tija ya uwekezaji wao.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya uwekezaji ili kukagua, kusikiliza na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika uwekezaji wao. Waziri Kairuki alitembelea Kampuni inayojishughulisha na kilimo cha Mpunga ya Highland Estate iliyopo katika Kata ya Ubaruku Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya Juni 26, 2020.

Akiwa katika ziara hiyo, Waziri Kairuki amewataka wawekezaji wote nchini kuwajibika katika jamii zinazowazunguka ili kuendelea kuwa na mchango chanya kwa jamii kwani kufanya hivyo kutaboresha mahusiano mazuri kati yao na jamii inayowazunguka.

“Tunawashuru kwa namna mnavyowajibika katika jamii, huo ndiyo uwekezaji tunaoutaka, pamoja na nyie kupata faida ni vyema kuwajibika katika jamii inayowazunguka, jamii ambayo uwekezaji wako upo, tumeelezwa maeneo mengi ambayo mmetoa mchango wenu zikiwepo shule, kuchangia huduma za afya, mnavyojenga mabanio mapya, ujenzi wa kituo cha polisi na mengine mengi.”alisema Mhe. Kairuki

Aidha alibainisha mikakati ya Serikali katika kuhakikisha inaboresha mazingira ya wawekezaji na wafanyabiashara nchini hivyo ni vyema kuzitambua na kuunga mkono jitihada hizo kwa vitendo na kuzikumbuka jamii zetu.

ADVERTISEMENT

“Serikali kwa sasa inaendelea kuboresha mazingira bora ya biashara na uwekezaji, na kwa upande wa kilimo hii ni sekta ambayo tunaipa kipaumbele sana tukitambua kuwa ni sekta inayoajiri watu wengi lakini inamnyororo mrefu wa thamani na wanufaika ni wengi” alisema Waziri Kairuki

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa shamba hilo Bw. Sadiki Wigira alisema kuwa, sambamba na uzalishaji wa mpunga, kampuni inajishughulisha na kilimo cha Matunda, Mbogamboga, zao la korosho, ufugaji wa ng’ombe wa maziwa pamoja na ng’ombe wa nyama na vilevile wanamatarajio ya kuanzisha Kiwanda cha kusindika nyama na maziwa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bw. Aswege Kaminyoge amemshuruku Waziri Kairuki kwa kufanya ziara katika Wilaya hiyo na kutembelea kampuni ya Highland Estate kwani Kampuni hiyo pamoja na kampuni zingine zilizopo hapa zimekuwa zikitoa ushirikiano mzuri kwa Serikali kwa kulipa kodi zote za Halmashauri bila usumbufu na amewataka kuendelea kushirikiana ili kuboresha uchumi wa nchi yetu.

Mhe. Waziri Kairuki ameipongeza kampuni ya Highland Estate kwa uwekezaji walioufanya katikka eneo la Mbarali kwani uwekezaji huo umetoa ajira kwa wakulima zaidi ya 4,000 wa makundi mbalimbali pamoja na ajira za kudumu zaidi ya 310.

Vilevile zaidi ya wakulima 20,000 wamenufaika katika huduma mbalimbali zikiwemo huduma za ugani, mafunzo, vitendea kazi, pembejeo za kilimo, mbinu bora za kilimo pamoja na fursa za ardhi yao kwa wakulima wadogowadogo ambao hawamiliki ardhi.

Jensen Kato

Jensen Kato

Next Post

TAASISI YA NEW FACE CREATIVES YAIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

Discussion about this post

Habari Mpya

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

by Pesatu Reporter
June 23, 2022
0

Mapendekezo yamepitishwa kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) leo 23...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In