Home BIASHARA Wafugaji watakiwa kubadilika

Wafugaji watakiwa kubadilika

0 comment 114 views
Na Mwandishi wetu

Baada ya kuzindua kiwanda cha kusindika mazao yatokanayo na mifugo ambacho kinamilikiwa na wanawake katika kijiji cha Ololosokwani wilaya ya Ngorongoro, kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Hamad Amour ameshauri wafugaji kujenga makazi bora na kuondokana na mazingira duni wengi wanayoishi hivi sasa.

Amesema haina maana ya kuwa na mifugo mingi kama watu hao bado wanaendelea kuishi katika dimbwi kubwa la umaskini hivyo amewasisitiza kubadilika na kuanza ufugaji wa mifugo michache ambayo ili wapate kunufaika nayo.

Mbali na hayo, pia amewataka wafugaji kufuga kitaalamu zaidi, jambo ambalo litawainua wao kiuchumi na pia litasaidia kuondoa migogoro ya mara kwa mara kati yao na wakulima.

Amepongeza kikundi hicho cha wanawake wajasiriamali kwa kuanzisha kiwanda ambacho kinajishughulisha na kuzalisha bidhaa zinazotokana na kwato, ngozi na pembe za wanyama ambazo zinawasaidia kujiajiri wenyewe na kuboresha maisha yao kwa ujumla.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter