Home KILIMO Bei ya kakao yafika 8,079 kutoka 4,611 mwaka 2018/19

Bei ya kakao yafika 8,079 kutoka 4,611 mwaka 2018/19

0 comment 200 views

Bei ya zao la kakao imeongezeka kutoka Sh Sh 4,611 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 hadi kufikia Sh 8,079 Oktoba kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde ameeleza kupanda kwa bei ya zao hilo Novemba 7, 2023 Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kyela Ally Jumbe Mlaghila kuhusu mfumo wa uuzaji wa zao la Kakao ili kumnufaisha mkulima baadala ya wafanyabiashara wachache.

Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde.

Akijibu swali hilo, amesema bei ya zao hilo imekuwa ikiimarika ukilinganisha na miaka iliyopita.

“Wastani wa bei ya Kakao kwa kilo kuanzia msimu wa 2018/2019 ilikuwa Sh 4,611 na mwaka wa fedha 2019/2020 ilikuwa Sh 5,034, na 2020/2021 ilikuwa Sh 4,818 ambapo mwaka wa fedha 2021/2022 ilikuwa 4,711.

Hadi kufikia tarehe 23 Oktoba msimu wa mwaka wa fedha 2023/2024 wastani wa bei ya Kakao kwa kilo imefikia shilingi 8,079,” ameeleza Silinde.

Silinde ameeleza kuwa zao la Kakao huuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani chini ya utaratibu wa minada ambao huratibiwa na Vyama vya Ushirika.

Mfumo huo ulianza kutumika mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo bei ya Kakao imeendelea kuimarika kulingana na hitaji la soko.

Ameeleza kuwa serikali kupitia Wizara ya Kilimo itaendelea kuimarisha mifumo ya uuzaji wa mazao nchini ili kuongeza ushindani na kumnufaisha mkulima.

Aidha , Silinde amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya uwekezaji katika zao la kahawa nchini na itaendelea kuwasaidia wakulima katika maeneo yote nchini yanayolima zao hilo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter