Home VIWANDAUZALISHAJI Watanzania washauriwa kuwekeza kwenye misitu

Watanzania washauriwa kuwekeza kwenye misitu

0 comment 162 views

Watanzania wametakiwa kuwekeza katika misitu na kushiriki katika ufugaji nyuki kwa kuzingatia njia sahihi zilizofanyiwa utafiti ili wapate tija katika rasilimali za misitu zilizopo nchini.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Matumizi ya Misitu Dkt. Chelestino Balama wakati akiongea na baadhi ya timu ya wataalamu wa misitu na nyuki na waandishi wa habari waliofika ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Mkoani Morogoro na kutembelea baadhi ya tafiti zinazofanywa.

“Sisi kama taasisi ya TAFORI tunafanya tafiti ambazo ni kwa ajili ya kuboresha vipato kwa jamii lakini pia kwa ajili ya kuboresha uchumi wa nchi yetu.

Mojawapo ni tafiti ya kuzalisha miti katika maeneo mbalimbali ili kuwa na taarifa sahihi za miti anbayo inafaa kupandwa katika eneo fulani ambapo vijana wengi wamejikita huko na imekuwa ni sehemu ya ajira,” amesema Balama.

Ameeleza kuwa taasisi hiyo imefanya utafiti ambao unahusika na kuangalia rasilimali za misitu ikiwemo kuona ni namna gani zinachangia kwenye kuokoa malighafi katika viwanda vya misitu hapa nchini na utafiti huu umekuwa na mchango mkubwa kwenye kuleta ajira kwa vijana, kwa kuwa wamejikita kuanzia kwenye mnyororo mzima wa mazao ya misitu.

Afisa Mtafiti Mkuu kutoka TAFORI ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi tafiti ya uzalishaji Misitu Dkt. Stephen Maduka ambaye amebainisha uwepo wa bustani ya miti ya Utafiti ya TAFORI iliyopo pfisini kwao kwa lengo mahususi ya kufanya utafiti katika kunusuru miti ya asili isitoweke ikiwemo mti wa Mkurungu, Msandali na Msekeseke inayovunwa kwa wingi kwa ajili ya biashara ya utengenezaji wa samani.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkurugenzi ya Utafiti wa Ufugaji Nyuki TAFORI Bw. Allen Kazimoto amewataka Vijana na Wanawake kushiriki kikamilifu katika ufugaji nyuki kwa kuzingatia ubora wa mazao ya nyuki yanayokidhi soko la ndani na pia la Kimataifa ili waweze kupata tija katika ufugaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter