Home VIWANDAMIUNDOMBINU ERB yafuta usajili wa mamia ya wahandisi nchini

ERB yafuta usajili wa mamia ya wahandisi nchini

0 comment 144 views
Na Mwandishi wetu

Naibu Msajili wa Bodi ya Wahandisi Nchini (ERB) Mhandisi Patrick Barozi amesema wahandisi 407 na Kampuni za Wakandarasi 39 wamefutiwa usajili baada ya kugundulika kuwa na makosa mbalimbali. Barozi pia ametoa wito kwa serikali kutunga sheria itakayowezesha miradi mikubwa kutumika kama vituo vya mafunzo.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Ninatubu Lema ametaka serikali kupiga marufuku uingizaji wa bidhaa na vifaa vya ujenzi ambavyo vinaweza kuzalishwa ndani ili kusaidia ukuaji wa viwanda vya ndani. Amesema ni vizuri masharti yakawekwa kwa kampuni yoyote  ambayo itapewa mradi mkubwa hapa nchini ambayo yatalazimu kampuni hizo kushirikisha kampuni za kizalendo za hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema wahandisi hapa nchini wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa ubora ili kuepuka kero ambazo zimewahi kujitokeza miaka ya nyuma kama majengo kuanguka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter