Home KILIMO Mongella aomba Waziri Tizeba kuvunja Bodi ya Pamba

Mongella aomba Waziri Tizeba kuvunja Bodi ya Pamba

0 comment 63 views
Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ameomba Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charles Tizeba kuvunja Bodi ya Pamba kanda ya ziwa kwa kushindwa kutelekeza majukumu yake kama inavyotakiwa na kusema bodi hiyo imekuwa kikwazo katika harakati za kilimo cha pamba nchini hivyo kuwakatisha tama wakulima wa zao hilo.

Mongela ametaka mamlaka husika kuchukua hatua za haraka akidai bodi hiyo imekuwa ikisababisha kilimo cha pamba kuendelea kuwa cha chini na hivyo kuikosesha serikali mapato. Amelalamikia bodi hiyo kwa vitendo vya kuchelewa kupeleka mbegu na dawa muhimu kwa wakulima, hali inayopelekea mavuno ya pamba kupungua katika wilaya mbalimbali mkoani humo.

Mbali na hayo,Mkuu huyo wa Mkoa pia ameagiza bodi ya pamba kuhakikisha kuwa wakulima wa zao hilo wanapelekewa mbegu za pamba hadi kufikia mwisho wa mwezi huu akionya kuwa hatua nyingine zitachukuliwa dhidi yao endapo watashindwa kufanya hivyo.

Uzalishaji wa zao la pamba katika mkoa wa Mwanza umekuwa ukishuka katika miaka ya hivi karibuni hadi kufikia tani 5,037.43 pekee katika msimu wa kilimo wa mwaka 2015/2016.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter