Home VIWANDANISHATI STAMICO yaja na kampeni kabambe wiki ya nishati nchini

STAMICO yaja na kampeni kabambe wiki ya nishati nchini

0 comment 14 views

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewaalika wananchi kushiriki kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia katika Wiki ya Nishati Safi ya Kupikia ya Rafiki Briquettes yenye kauli mbiu ya “Zima Mkaa wa Miti na Kuni, washa Rafiki Briquettes” iliyoandaliwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)

Akiongea kuhusu kampeni hiyo kabambe inayotarajiwa kuanza Desemba 20 hadi 22, 2024 katika Mkoa wa Dar es Salaam, RC Chalamila amesema kwa kushirikiana na STAMICO wameandaa kampeni kabambe ambayo itahamasisha wananchi kutumia Nishati safi ya kupikia ambayo ni mkaa uliotengenezwa kwa teknolojia kubwa inayotumia malighafi ya makaa ya mawe.

Amehamasisha wakazi wa Mkoa huo kujenga tabia ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia ambayo ndiyo dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kinara Barani Afrika katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Ameitaka kampeni hiyo ya nishati safi ifanyike kwa ukubwa wake ili kuhakikisha wana Dar es Salaam wanapata uelewa na maarifa ya kutosha juu ya matumizi ya nishati hiyo hususani hatua zilizotumika kuifanya bidhaa hii kutokuwa na hewa hatarishi.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwapongeza STAMICO kwa kuamua kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia jambo linalochukuliwa kama mkakati namba moja katika jitihada za Serikali kuanza kupunguza matumizi ya mkaa utokanao na kuni.

“Niwapongeze STAMICO kwa kutengeneza bidhaa ambayo inaleta chachu ya kuhamasisha matumizi nishati safi ili kuondokana na nishati zenye athari kwa watumiaji,” alisema RC Chalamila.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse amesema kampeni hii inayotarajiwa kuanza Desemba 20, 2024 hadi Desemba 22, 2024 ili kuweza kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi kwa wananchi.

Amesema Shirika limebuni teknolojia ya kutengeneza mkaa kwa kutumia malighafi ya makaa ya mawe ili kuunga mkono juhudi za Rais za matumizi ya Nishati safi ya kupikia kwa watanzania tena kwa bei nafuu ambayo kila mtanzania anaweza kuimudu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter