Home WANAWAKE NA MAENDELEO Rais Dkt. Mwinyi ahimiza wanawake kugombea nafasi za uongozi

Rais Dkt. Mwinyi ahimiza wanawake kugombea nafasi za uongozi

0 comment 10 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi muda utakapowadia.

Rais Dkt. Mwinyi ametoa rai hiyo Machi 06, 2025 katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika Viwanja vya Maonesho Dimani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dkt. Hussein Mwinyi akiwa ameongozana na mkewe Mariam Mwinyi pamoja na viongozi wengine katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa za kiuchumi kupitia sera na mipango mbalimbali ya uwezeshaji huku akiwahimiza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa kupitia Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi ZEEA wanufaika 34,746 wamefikiwa kati yao 17,811 ni wanawake waliochangia asilimia 51.2 ya wanufaika wote.“Serikali kupitia Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi imewezesha utoaji wa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilionii 34.9 ambapo Shilingi bilioni 21 sawa na asilimia 60 zimeelekezwa kwa wanawake,” ameeleza Rais Dkt. mwinyi.

Aidha, ametoa agizo kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Wizara inayoratibu masuala ya Majukwaa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda na wadau wote kuandaa utaratibu wa kuhuwisha Majukwaa ya Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi ili yalete matokeo yaliotarajiwa.

Vilevile Rais Dkt. Mwinyi amezindua Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wa 2025-2030 pamoja na Muongozo wa Uanzishwaji wa Majukwaa na Uendeshaji wa Majukwaa ya Wanawake.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter