Home BIASHARA Emirates iliyotua ghafla Dar yaleta baraka

Emirates iliyotua ghafla Dar yaleta baraka

0 comment 125 views

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari amesema kuwa ndege kubwa aina ya Airbus A380-800 ya Shirika la Ndege la Emirates iliyotua ghafla katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Aprili 25 ilipelekea biashara uwanjani hapo pamoja na mahotelini kuongezeka.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa mbali na faida hizo pia serikali nayo imeweza kupata mapato kutokana na kuuza mafuta takribani lita 98,000 kwa shirika hilo. Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 475 pamoja na wahudumu 27 ilikuwa safarini kuelekea nchini Mauritius lakini ililazimika kutua ghafla Dar es salaam kutokana na hali mbaya ya hewa.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) Joseph Nyahade amesema kuwa mamlaka zote ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara ya Uhamiaji zimeingiza mapato ya ghafla kutokana na ndege hiyo kutua ghafla hapa nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter