Home VIWANDAMIUNDOMBINU Bilioni 17 kutumika katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Karume

Bilioni 17 kutumika katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Karume

0 comment 111 views

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mustafa Aboud Jumbe amesema takribani Sh. 17 bilioni zitatumika katika upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume. Katibu huyo amesema fedha hizo ni mkopo kutoka China na sehemu nyingine ya mradi huo inasimamiwa na serikali ya Tanzania.

Jumbe ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo, kutatkuwepo na fursa mbalimbali za biashara sambamba na ukuaji katika sekta ya utalii visiwani humo kwani uwanja huo mpya utakuwa na uwezo wa kupokea ndege za kiwango cha juu tofauti na hali ilivyo sasa. Vilevile ametoa wito kwa vijana zaidi kujikita katika masomo ya anga kwani kutakuwa na fursa nyingi za ajira punde baada ya mradi huo kumalizika.

Kwa upande wake, Mshauri Mwelekezi wa kampuni ya Beijing Construction Engineering Group ambayo inajenga uwanja huo Leguin Manc amehakikisha ujenzi huo utakamilika katika muda waliokubaliana ili kuepuka usumbufu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter