Home KILIMO Kilimo cha Alizeti kinalipa

Kilimo cha Alizeti kinalipa

0 comment 160 views

Ukizungumzia mazao muhimu ya biashara basi bila shaka, lazima utazungumzia zao la alizeti. Zao hili limechangia kwa kiasi kikubwa kuwainua wakulima kiuchumi na kuongeza pato la taifa. Mbegu za alizeti hutengeneza mafuta ambayo yanatumika kupitia wakati makapi yanayotokana na mbegu hizo ni chakula bora kwa mifugo. Kwa mujibu wa takwimu kutoka  kitengo cha mbegu za mafuta katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mbeya, mkulima anaweza kuvuna hadi magunia matano ya alizeti katika hekta moja ya shamba.

Alizeti hulimwa kwa wingi mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Rukwa pamoja na Manyara. alizeti hutegemea sana hali ya hewa ya eneo husika. Maeneo yenye mvua nyingi, zao la alizeti hupandwa mwishoni mwa Januari hadi katikati ya Februari, wakati katika maeneo yenye mvua kidogo mkulima anaweza kupanda kuanzia mwezi Desemba hadi katikati ya mwezi wa kwanza.

Adui mkubwa wa kilimo hiki ni ndege ambao huweza kuteketeza hadi asilimia 50 ya mazao yote shambani, mara nyingi inashauriwa kutopanda alizeti karibu na msitu au pori kwasababu ya uwepo wa ndege. Mkulima anayefanya au anayetarajia kufanya kilimo hiki anapaswa kuwa na mbinu mbadala ya kuepuka mashambulizi ya ndege. Wengi hutumia sanamu, makopo au hukaa na kufukuza makundi ya ndege wenyewe. Bila ya kuweka ulinzi shambani kwako, ndege wanaweza kuharibu mazao yako yote. Mbali na ndege, aina hii ya kilimo pia huweza kushambuliwa na magonjwa mengine kama vile madoa ya majani, kuoza kwa mizizi na hata virusi.

Ili kuepukana na magonjwa ya aina hiyo, ni vizuri kufanya kilimo cha mzunguko wa mazao, kupanda mbegu safi ambazo zimethibitishwa na wataalamu, kuchoma masalia kila baada ya msimu kumalizika na kutumiwa dawa kuua wadudu endapo mazao yako yataonyesha dalili ya kudhoofika. Ni muhimu kutafuta wataalamu wa masuala ya kilimo pale unapohitaji msaada.

Alizeti ni zao zuri sana la biashara na wakulima wengi zaidi wamekuwa wakijitika katika aina hii ya kilimo. Japokuwa uwekezaji katika zao hili umekuwa mdogo tofauti na mazao mengine, kilimo hiki kimeonyesha mafanikio makubwa hapa nchini. Wakulima wanatakiwa kuacha kufanya kilimo cha mazoea na kuwekeza zaidi katika mazao haya ya biashara ambayo yana faida kubwa zaidi sio kwao tu bali kwa taifa. Sekta ya kilimo inabadilika hivyo wakulima wanatakiwa kufikiria kufanya kilimo cha biashara na kujiendeleza kiuchumi.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter