Home BIASHARA TRA yakamata bidhaa za magendo Arusha

TRA yakamata bidhaa za magendo Arusha

0 comment 110 views

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema mamlaka hiyo imekamata magari mawili mkoani Arusha yaliyokuwa na bidhaa za magendo zenye thamani ya takribani Sh.20 milioni. TRA imetaja bidhaa zilizokamatwa kuwa ni pamoja na sukari na mafuta ya kupikia ambazo zilitakiwa kulipiwa kodi ya Sh.28.5 milioni lakini kutokana na kusafirishwa kimagendo, wamiliki wake sasa watalazimika kulipa Sh. 39.2 milioni kama kodi na faini ya kutofuata taratibu na sheria.

Kamishna Kichere ametoa wito kwa wananchi kufuata taratibu za uingizaji wa bidhaa ili kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza kwani mamlaka hiyo haitovumilia vitendo vya aina hiyo na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote watakaovunja sheria.Kichere pia amesisitiza kuwa, zoezi la kukamata bidhaa zinazoingizwa nchini kwa njia za magendo ni endelevu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter