Home BENKI Mkombozi yaongeza gawio la wanahisa

Mkombozi yaongeza gawio la wanahisa

0 comment 123 views

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Mkombozi Method Kashonda amesema gawio la wanahisa wa benki hiyo limeongezeka kutoka Sh. 20 na kufikia Sh. 25. Kashonda ameongeza kuwa malipo hayo yatafuata taratibu zilizowekwa na Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE) na yatafanyika kuanzia Julai 6 baada ya taratibu zote kukamilika.

Mwaka jana, ongezeko la amana za wateja ambalo lilichangia kwa kiasi kikubwa  katika ufanisi wa benki hiyo lilifikia Sh. 121.12 bilioni kutoka Sh. 102.55 bilioni ambayo ni sawa na asilimia 18 huku mikopo nayo ikiongezeka kwa asilimia 10.8.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, George Shumbusho ameeleza kuwa benki ya Mkombozi imejipanga kutekeleza miradi mbalimbali katika jamii ikiwemo miundombinu ili kukabiliana na mahitaji ya hivi sasa na hata baadae.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter