Home BIASHARAUWEKEZAJI Alliance One yazindua mpango wa upandaji miti Kasulu

Alliance One yazindua mpango wa upandaji miti Kasulu

0 comment 215 views

Kasulu, Kigoma

Alliance One yazindua mpango wa upandaji miti Kasulu

“Ustahimilivu katika urejeshaji wa misitu na maendeleo katika maisha ya jamii.”

Kigoma, Jumanne, 26 Juni 2018. Alliance One Tobacco Tanzania Limited, (AOTTL) kwa ushirikiano na Imperial Tobacco (IT) imezindua kampeni ya upandaji miti wilayani Kasulu, mkoa wa Kigoma, katika jitihada ya kusisitiza uwezekano wa kurejesha misitu Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mh. Brig. Jen. Emmanuel Maganga, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Alliance One, Hamis Liana alisema, “mpango huu wa upandaji miti ni wa kimapinduzi na unaochochea urejeshaji endelevu wa misitu na maendeleo katika jamii”.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mh. Brig. Jen. Emmanuel Maganga aliwapongeza Alliance One kwa mpango huo akisema, “Serikali inathamini ushiriki wa jamii katika kampeni hii na uboreshaji wa jumla kwa mkoa. Nimejitoa kusimamia kampeni hii ili kuhakikisha ushiriki kamili wa jamii na muendelezo wa mpango huu”.

Mradi huu unalenga kuwaonyesha wadau muhimu katika sekta za umma na binafsi, na jamii kwa ujumla; kwamba kupitia mipango stahiki na kujitoa, urejeshaji misitu nchini Tanzania unafikiwa.

“Mradi wa kupanda miti Kasulu ulianza mwaka 2014, hadi sasa, hekta 565 zimepandwa na idadi kubwa ya wanajamii wamenufaika kutokana na mradi huu” aliongeza Bw. Laina. Alliance One inafanya kazi na wamiliki 37 wa ardhi kwa sasa, 21 kati yao wakiwa ni wakulima. Miti iliyopandwa inatarajiwa kukomaa baada ya miaka 7 na inakadiriwa itazalisha mapato kufikia Shilingi bilioni 1.9.

Alliance One inalenga kushirikiana na jamii pamoja na taasisi, kama shule, na makanisa ikitoa msaada wa ujuzi wa kilimo na kifedha kwa kuboresha mazingira lakini pia kujenga kipato cha jamii kwa kuwekeza kwaajili ya siku zijazo.

 Alliance One Tobacco Tanzania Limited ni kampuni tanzu chini ya kampuni mama ya Alliance One International, kampuni kubwa ya kujitegemea inayofanya biashara  ya tumbaku. Alliance One ni moja ya mitandao mikubwa ya wakulima, wanunuzi, wasindikaji na wasambazaji wa tumbaku.

Alliance One ni matokeo ya muungano wa DIMON Incorporated na Standard Commercial Corporation, makampuni yote yakiongoza katika kuuza tumbaku yenye ubora wa hali ya juu na huduma bora kwa wateja. Hivyo, Alliance One imejumuisha zaidi ya miaka 200 ya uzoefu na ujuzi, ikizaa mshindani wa kipekee mwenye dira inayolenga wateja wake, pamoja na maono ya baadaye.

Zaidi ya kununua, kusindika na kuuza tumbaku, pia hutoa mafunzo ya kilimo na msaada wa kifedha kwa uzalishaji wa  tumbaku.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter