• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Wednesday, February 8, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Alliance One yazindua mpango wa upandaji miti Kasulu

Patricia Richard by Patricia Richard
June 29, 2018
in UWEKEZAJI
0
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Louis Bura akipanda mti kuadhimisha uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa na kampuni ya Alliance One Tobacco mkoani kigoma hivi karibuni. Wengine ni wataalamu wa misitu kutoka Alliance One.

Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Louis Bura akipanda mti kuadhimisha uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa na kampuni ya Alliance One Tobacco mkoani kigoma hivi karibuni. Wengine ni wataalamu wa misitu kutoka Alliance One.

Share on FacebookShare on Twitter

Kasulu, Kigoma

Alliance One yazindua mpango wa upandaji miti Kasulu

ADVERTISEMENT

“Ustahimilivu katika urejeshaji wa misitu na maendeleo katika maisha ya jamii.”

Kigoma, Jumanne, 26 Juni 2018. Alliance One Tobacco Tanzania Limited, (AOTTL) kwa ushirikiano na Imperial Tobacco (IT) imezindua kampeni ya upandaji miti wilayani Kasulu, mkoa wa Kigoma, katika jitihada ya kusisitiza uwezekano wa kurejesha misitu Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mh. Brig. Jen. Emmanuel Maganga, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Alliance One, Hamis Liana alisema, “mpango huu wa upandaji miti ni wa kimapinduzi na unaochochea urejeshaji endelevu wa misitu na maendeleo katika jamii”.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mh. Brig. Jen. Emmanuel Maganga aliwapongeza Alliance One kwa mpango huo akisema, “Serikali inathamini ushiriki wa jamii katika kampeni hii na uboreshaji wa jumla kwa mkoa. Nimejitoa kusimamia kampeni hii ili kuhakikisha ushiriki kamili wa jamii na muendelezo wa mpango huu”.

Mradi huu unalenga kuwaonyesha wadau muhimu katika sekta za umma na binafsi, na jamii kwa ujumla; kwamba kupitia mipango stahiki na kujitoa, urejeshaji misitu nchini Tanzania unafikiwa.

“Mradi wa kupanda miti Kasulu ulianza mwaka 2014, hadi sasa, hekta 565 zimepandwa na idadi kubwa ya wanajamii wamenufaika kutokana na mradi huu” aliongeza Bw. Laina. Alliance One inafanya kazi na wamiliki 37 wa ardhi kwa sasa, 21 kati yao wakiwa ni wakulima. Miti iliyopandwa inatarajiwa kukomaa baada ya miaka 7 na inakadiriwa itazalisha mapato kufikia Shilingi bilioni 1.9.

Alliance One inalenga kushirikiana na jamii pamoja na taasisi, kama shule, na makanisa ikitoa msaada wa ujuzi wa kilimo na kifedha kwa kuboresha mazingira lakini pia kujenga kipato cha jamii kwa kuwekeza kwaajili ya siku zijazo.

 Alliance One Tobacco Tanzania Limited ni kampuni tanzu chini ya kampuni mama ya Alliance One International, kampuni kubwa ya kujitegemea inayofanya biashara  ya tumbaku. Alliance One ni moja ya mitandao mikubwa ya wakulima, wanunuzi, wasindikaji na wasambazaji wa tumbaku.

Alliance One ni matokeo ya muungano wa DIMON Incorporated na Standard Commercial Corporation, makampuni yote yakiongoza katika kuuza tumbaku yenye ubora wa hali ya juu na huduma bora kwa wateja. Hivyo, Alliance One imejumuisha zaidi ya miaka 200 ya uzoefu na ujuzi, ikizaa mshindani wa kipekee mwenye dira inayolenga wateja wake, pamoja na maono ya baadaye.

Zaidi ya kununua, kusindika na kuuza tumbaku, pia hutoa mafunzo ya kilimo na msaada wa kifedha kwa uzalishaji wa  tumbaku.

 

Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post

Walemavu na wenye mahitaji maalum wapatiwe fursa sawa

Discussion about this post

Habari Mpya

Hewa ukaa, eneo jipya la uwekezaji Tanzania

February 7, 2023

Halmashauri zahamasishwa kutenga maeneo kwa ajili ya vijana

February 7, 2023
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji.

Kijaji: changamkieni fursa za biashara Afrika

February 6, 2023
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi

Rais Mwinyi aonya wafanyabiashara

February 6, 2023
Baadhi ya vijana wakiwa kwenye Kongamano la Vijana wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati lijulikanalo kama ‘University Ladies and Gentlemen Conference.

Vijana wahamasishwa kuchangamkia fursa za kilimo

January 31, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki.

Halmashauri Tanzania zakusanya 485.42 bilioni

January 31, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Hewa ukaa, eneo jipya la uwekezaji Tanzania

by Pesatu Reporter
February 7, 2023
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana amewakaribisha wawekezaji kufanya biashara ya hewa ukaa na Serikali ya Tanzania. Dkt....

Halmashauri zahamasishwa kutenga maeneo kwa ajili ya vijana

by Pesatu Reporter
February 7, 2023
0

Halmashauri za Wilaya nchini zinahamasishwa kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya mashamba ya pamoja (Block Farm) kwa ajili ya kuwezesha...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In