Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro William Olenasha amesema hadi kufikia mwaka 2019, vijiji 35 vitakuwa vimepata umeme wa REA III na baadae wataendelea na maeneo mengine. Waziri Olenasha ameyasema hayo katika kijiji cha Sakala alipofanya mkutano wa hadhara na wananchi na kusema kuwa, kila nyumba lazima itapata umeme na kuwasihi wananchi kuonyesha mwitikio mkubwa na kuichangamkia fursa hiyo yenye kuleta maendeleo.
Olenasha amesema kuwa tayari nguzo za umeme zimeendelea kupita katika maeneo mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha Ngorongoro inabadilika kuanzia miundombinu iliyopo mpaka mazingira ya watu ili kuhakikisha wanajenga Ngorongoro mpya.
“ Wote ni mashahidi hili hatuzungumzi tena, sio hadithi nguzo tayari zinasambaa katika vijiji na tunategemeaifikapo mwaka 2019 vijiji 35 vitakuwa na umeme.” Alisema Olenasha.
Kufuatia ziara hiyo, wananchi wamempongeza mbunge huyo kwa kuendelea kutekeleza ahadi zake na kuleta maendeleo.