Home BIASHARAUWEKEZAJI Wachimbaji wadogo kuwezeshwa

Wachimbaji wadogo kuwezeshwa

0 comment 111 views

Naibu Waziri wa madini Dotto Biteko amesema Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewatangazia wachimbaji wadogo wa madini wanaofuata sheria kwa kulipa kodi stahiki ambayo husaidia katika upatikanaji wa mikopo ya vitendea kazi kuwa, watapatiwa leseni na kumilikishwa maeneo ya uchimbaji kutokana na wawekezaji wakubwa kushindwa kuyaendeleza kwa lengo la kuinua uchumi wa taifa na kupunguza umaskini.

 

Biteko amesema hayo alipotembelea mgodi wa Bingwa Reef wilayani Geita wakati akijibu baadhi ya malalamiko ya wachimbaji wadogo wadogo katika eneo hilo.

 

Katika ziara yake, Naibu Waziri Biteko pia amepata nafasi ya kutembelea kiwanda cha kisasa cha uchenjuaji madini ya dhahabu cha CIP ambacho husaga na kuchuja takribani tani 1000 za mchanga kwa siku. Akiwa katika eneo hilo, wachimbaji wameeleza changamoto zilizopo katika upatikanaji wa mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na kusisitiza kuwa endapo watapatiwa mikopo hiyo, wataongeza uzalishaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter