Home BIASHARAUWEKEZAJI TIC yawapa somo wajasiriamali

TIC yawapa somo wajasiriamali

0 comment 95 views

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetoa wito kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kuchangamkia fursa za uwekezaji. Meneja wa kituo hicho kanda ya kaskazini Daudi Riganda amesema hayo wakati wa utoaji elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali katika maonyesho ya nanenane yanayoendelea.

Meneja huyo ameongeza kuwa elimu wanayotoa itawasaidia wawekezaji pamoja na wajasiriamali wa ndani kuelewa wanavyoweza kuhudumiwa na kituo hicho na kufahamu taratibu za kupata vibali na leseni za biashara. Mbali na hayo, amefafanua kuwa watu wengi wanadhani dhana nzima ya uwekezaji inawajali zaidi watu wa ndani, madai ambayo amesema hayana ukweli wowote.

“Uwekezaji sio wa nje tu watanzania wamechangamkia fursa za uwekezaji na kusajili miradi yao kwa sekta mbalimbali tofauti na inavyodhaniwa”. Amesema Riganda.

Akizungumzia maonyesho ya nanenane yanayoendelea, Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga amewataka wananchi wa ukanda huo kujitokeza kwa wingi na kujifunza namna ambazo zinaweza kuwasaidi kufanikiwa katika sekta mbalimbali na kuongeza uchumi wao. Amewataka wajasiriamali kutumia maonyesho haya kufaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter