Serikali imetenga jumla ya kiasi cha Sh. 210 bilioni kwa ajili ya kukarabati upya mradi wa maji wa Handeni Trunk Main (HTM) ili kuboresha huduma ya maji kutoka Korogwe hadi Handeni mkoani Tanga. Akizungumza na wakazi wa kata ya Msasa, Mbunge wa jimbo la Handeni Mjini Omar Kigoda amesema serikali imetenga kiasi hicho cha fedha ili kuboresha mradi huo wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa maji ya uhakika kwa wakazi wa jimbo hilo na wilaya kwa ujumla.
Soma Pia Bila maji, uchumi wa viwanda ni ndoto
Uhitaji mkubwa wa huduma ya maji ikiwa na matokeo ya ongezeko la watu katika wilaya ya Handeni, imetajwa na Mbunge huyo kuwa sababu kuu iliyofanya mtangulizi kupeleka ombi la kurekebisha na kuboresha mradi huo ulioanzishwa mwaka 1974 wakati wakazi wa Handeni wakiwa wachache.
“Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wilaya ya Handeni inaonyesha kuwa na jumla ya wakazi 355,702 hadi sasa idadi hiyo itakuwa imeongezeka nakuna ulazima wa kuuboresha mradi huo”. Amesema Kigoda
Aidha, Kigoda amesema licha ya serikali kutoa kiasi hicho cha pesa imeweza pia kutoa Sh. 277 milioni kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya maji iliyopo kwenye mji huo ili kuwaondolea wananchi kero hiyo ya muda mrefu.
Soma Pia Tabora kunufaika na mradi wa maji