Home VIWANDAUZALISHAJI TFS kuinua wazalishaji wa asali

TFS kuinua wazalishaji wa asali

0 comment 120 views

Wakati serikali ikichukua hatua kadhaa kuongeza uzalishaji wa asali nchini, Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kanda ya kaskazini wamekutana na vikundi vya wazalishaji wa mazao yatokanayo na nyuki ikiwa ni katika kutekeleza mpango wake wa kuviwezesha vikundi hivyo kiuchumi kwa kuvipatia nyenzo za uzalishaji huo ikiwa ni pamoja na mizinga ya nyuki pamoja na mavazi maalum ya kurinia asali.

Soma Pia Warina asali walalamikia uharibifu wa mazingira

Akizungumza katika halfa ya ugawaji wa vifaa hivyo kwa vikundi vya uzalishaji wa bidhaa za nyuki zikiwemo kikundi cha Sifa Environmental Group, Meneja wa TFS Wilaya ya Hai Evaline Mboya amesema kuwa licha ya Tanzania kushika nafasi ya pili Afrika kwa uzalishaji wa asali na nta ikiongozwa na Ethiopia, bado anaamini uwezeshaji huu ulioanzishwa utaweza pia kuwavutia wawekezaji na taasisi binafsi kuona umuhimu wa kuwekeza katika nta na asali.

“Wakala anatambua mchango wa vikundi hivi katika utunzaji wa mazingira na ameahidi kuendelea kutoa vifaa hivi kila mwaka ambavyo vitasaidia katika uhifadhi wa mazingira, lakini hii ni fursa kwa wadau wengine kuwekeza katika uzalishai ili kuongeza, sio tu uzalishaji wa nta na asali bali pia ubora wa bidhaa za nyuki zinazokubalika unaokidhi viwango vya soko la kimataifa” . Amesema Mboya

Soma Pia Wajasiriamali Singida kusafirisha asali nje

Kwa upande wake, Afisa Nyuki wa wilaya hiyo Joyce Kombe ametoa shukrani zake kwa Wakala wa Huduma za Misitu baada ya vifaa hivyo kutolewa amewataka wazalishaji hao kutobweteka wakisubiria asali na badala yake, wajaribu kuchunguza mizinga yao mara kwa mara ili kujihakikishia uwepo wa asali ya kutosha.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter