Home FEDHAMIKOPO Milioni 30 kuwanufaisha wanawake,vijana

Milioni 30 kuwanufaisha wanawake,vijana

0 comment 142 views

Vikundi vya wanawake na vijana katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera vimefanikiwa kunufaika na mikopo ya jumla ya Tsh. Milioni 30 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 uliotolewa  na Idara ya maendeleo ya jamii ya halmashauri hiyo.

Soma Pia Wanawake washauriwa kutumia mikopo kujiendeleza

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Ofisa wa maendeleo ya jamii wa halmashauri hiyo, Joseph Lusatila amesema kuwa fedha hizo ni moja kati ya fungu linalotengwa na halmashauri kwa ajili ya asilimia 10 kwa vijana na wanawake.

Soma Pia Wajasiriamali kufaidika na mikopo NSSF

Lusatila amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali ya halmashauri ya Ngara ilikuwa na makadirio ya kukusanya Sh.103.5 bilioni lakini hadi kufikia Juni 30, 2017 walikuwa wamekusanya kiasi cha Sh.930.7 milioni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Aidan Bahama amesema serikali imekuwa ikitoa mikopo kwa vijana japokuwa wengi wao wamekuwa wakizitumia pesa hizo kwa matumizi yaliyo nje na mipango. Bahama ametoa wito kwa wanufaika wa mikopo hiyo kutumia pesa hizo kwa tahadhari kubwa.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter