Home VIWANDANISHATI Tanesco yasisitiza umeme unajitosheleza

Tanesco yasisitiza umeme unajitosheleza

0 comment 90 views

Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Dk. Tito Mwinuka amesema shirika hilo linazalisha umeme wa kutosha na kueleza kuwa, umeme unaozalishwa hivi sasa ni megawati 1517.47, huku matumizi yakiwa ni megawati 900. Mwinuka amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya shirika hilo kwa kamati  ya kudumu ya bunge ya nishati na madini.

Dk. Mwinuka ameongeza kuwa, shirika hilo linaendelea na jitihada za kuwaunganishia umeme wananchi, kazi ambayo inaenda  sambamba na kuimarisha mifumo ya usafirishaji na usambazaji wa umeme, kwa lengo la kupunguza matukio ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Jitihada hizo zimepelekea mapato ya shirika hilo kuongezeka kila mwaka na kuwezesha shirika hilo kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini kuanzia mwaka 2015/16.

“Mapato ya shirika yameendelea kuimarika, ambapo katika kipindi cha mwaka 2017/18, makusanyo yamekuwa ya wastani wa Sh. 38 hadi 39 bilioni kwa wiki kutoka wastani wa Sh. 34 bilioni katika mwezi Aprili, 2018”. Amefafanua Dk. Mwinuka.

Akizungumzia suala la deni la shirika hilo, Dk. Mwinuka, amedai kuna sababu mbalimbali zinazopelekea deni hilo kuongezeka, ikiwa ni pamoja na gharama kubwa za kuzalisha umeme kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi ya taifa, ambapo shirika hilo hulazimika kuzalisha umeme kwa wastani wa Sh.763 kwa uniti moja.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter