Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji wamwaga bilioni 57 Iringa

Wawekezaji wamwaga bilioni 57 Iringa

0 comments 172 views

Uwekezaji umeendelea kuongezeka wilayani Mufindi mkoani Iringa huku ikielezwa kuwa, kampuni tatu zimewekeza mitaji ya takribani Sh. 57 bilioni katika viwanda vya kuchakata magogo, nguzo za umeme, kuni na mkaa zitokanazo na pumba za mbao. Kampuni hizo zimetajwa kuwa ni Hongway International inayoshughulika na kuchakata magogo, Qwihaya inayotengeneza nguzo za umeme na WF Renewable Resources inayotengeneza mkaa na kuni.

 

Meneja Rasilimali Watu wa Hongway International Michael Mkamba pamoja na Meneja wa WF Renewable Resources Oscar Kaduma wamesema wanalenga kuongeza thamani ya mazao ya misitu, kupeperusha bendera ya Tanzania kwa kuzalisha bidhaa zenye hadhi ya kimataifa na vilevile kuzalisha ajira takribani 500 kwa watanzania.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amesema serikali itashirikiana kwa karibu na wawekezaji na pia itawalinda. Hapi pia ametoa wito kwa wawekezaji zaidi kuendelea kujitokeza kwani kuna uhaba wa viwanda vya kuchakata maboksi na vifungashio, ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa Iringa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!