Home VIWANDAMIUNDOMBINU SGR yatandikwa rasmi

SGR yatandikwa rasmi

0 comment 89 views

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua rasmi kazi ya kutandika reli ya kisasa (SGR) eneo la soga mkoani Pwani.Reli hiyo ya kisasa kutoka Dar es salaam hadi Morogoro yenye urefu wa kilomita 300 imeanza rasmi kutandikwa huku Waziri Kamwele akishuhudiwa na Naibu wake Mhandisi Atashasta Nditiye na Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania.

Aidha Dk. Kamwelwe amebainisha kuwa reli hiyo itatumia umeme na itakuwa na spidi ya kilomita 160 kwa saa na katika kilomita 300 za reli hiyo, kilomita 205 ni za umbali wa kawaida na kilomita 95 ni kwa ajili ya reli kupishana ambapo reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 17000 za mizigo kwa mwaka na mkandarasi anayejenga ni kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchini Uturuki huku mshauri mwelekezi ni kampuni kutoka Japan akisaidiana na kampuni ya kizalendo ya hapa nchini.

Utandikaji wa reli hiyo umeanza rasmi baada ya kuingia kwa reli kiasi cha tani 7250 zilizoagizwa na kufanikiw kuwasili wiki mbili zilizopita ambapo zitatumika katika kipande cha urefu wa kilomita 60 huku vifaa vingine kama mataruma yakizalishwa na kiwanda cha soga kilichopo mkoa wa pwani huku saruji na kokoto pia vikizalishwa hapa nchini.

Mwisho Dk. Kamwelwe amewasisitiza wananchi walipe kodi ili kufanikisha jitihada za Rais John Magufuli za kujenga viwanda ambapo fedha hizo zitasaidia nchi kutumia fedha za ndani kujenga reli na miradi mingine.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter