Home BIASHARAUWEKEZAJI Sekta ya maji yasaka wawekezaji

Sekta ya maji yasaka wawekezaji

0 comment 109 views

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ametoa wito kwa sekta binafsi nchini kuwekeza katika sekta ya maji ili kupanua wigo wa upatikanaji wake hususani kwa wananchi walioko maeneo ya vijijini. Aweso ametoa wito huo wakati akizungumza na wanahabari ambapo ameongeza kuwa, idadi ya watanzania imeongezeka ikilinganishwa na rasilimali maji zilizopo hivyo uwekezaji mkubwa unahitajika katika sekta hiyo na ili kutimiza lengo hilo, lazima kuwepo na fedha za kutosha.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema serikali itaendelea kuongeza bajeti ya sekta ya maji ili kufanikisha lengo lake la kuwafikishia maji wananchi wote hasa wa maeneo ya vijijini. Katika maelezo yake, Aweso amesisitiza kuwa serikali imepanga ifikapo mwaka 2020, asilimia 85 ya watanzania wawe wamefikiwa na huduma ya maji safi na salama.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo amesema ushiriki wa sekta binafsi katika sekta hiyo bado ni mdogo. Prof. Mkumbo ambapo pia ameshauri sekta binafsi kuwekeza zaidi katika sekta ya maji hasa kwenye ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter