Home KILIMO Dk. Tizeba azuia halmashauri kutoa vibali kununua kahawa

Dk. Tizeba azuia halmashauri kutoa vibali kununua kahawa

0 comment 102 views

Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba “amepiga stop” halmashauri zote nchini kutoa vibali kwa wafanyabiashara vya kununua kahawa kwa wakulima. Waziri Tizeba ametoa zuio hilo alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara wilayani Karagwe wakati wa muendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliyoanza siku chache zilizopita mkoani Kagera.

“Wafanyabiashara wa kahawa ili wanunue zao hilo walikuwa wanaenda kuomba kibali cha ununuzi kilichokuwa kinatolewa na halmashauri za wilaya, Hili jambo tumelitafakari na wenzangu wa wizara hususani watendaji pamoja na Bodi ya kahawa tumeona halina maana tena”. Ameeleza Dk. Tizeba.

Waziri Tizeba amesisitiza kuwa hakuna sababu ya wafanyabiashara kuomba vibali vya kununua kahawa kwenye halmashauri na badala yake, itajitosheleza kuwa na leseni ya biashara ya kahawa inayotolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania, jambo ambalo linawatambulisha wafanyabiashara kama walipa kodi.

“Sasa hivi tunaingia kwenye mfumo wa ushirika hivyo wafanyabiashara watanunua kahawa kupitia mfumo huo mahususi hivyo hakuna sababu ya kusumbuliwa na halmashauri kwa kupewa vibali”. Amesema Dk. Tizeba.

Akizungumza kuhusu kahawa ya madaraja ya chini, Waziri huyo amesema kuwa, kahawa hiyo imekuwa ikizuiliwa kuuzwa nje ya nchi kwa kipindi kirefu sasa. Kwa mujibu wa utafiti wa kubaini namna inavyotumika nchini imeonekana kuwa kahawa hiyo hununuliwa na watu wachache ambao wanaratibu utaratibu wa kuuza nje huku waliokoboa wakizuiwa kuuza nje.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter