Home FEDHA TRA yakusanya trilioni 3.8 ndani ya miezi mitatu

TRA yakusanya trilioni 3.8 ndani ya miezi mitatu

0 comment 104 views

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) amesema mamlaka hiyo imekusanya Sh. 3.84 trilioni kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwaka wa fedha 2018/19, kuanzia Julai hadi Septemba 2018 ikilinganishwa na Sh. 3.65 trilioni ambazo zilikusanywa katika mwaka wa fedha wa 2017/18, Kayombo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, kiasi hicho ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.32.

“Katika mwezi Julai, 2018, TRA ilikusanya jumla ya Shilingi trilioni 1.20 sawa na ukuaji wa asilimia 9.20, mwezi Agosti, 2018 jumla ya Shilingi trilioni 1.27 zilikusanywa ikiwa ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.86 wakati mwezi Septemba, 2018 Mamlaka ilikusanya jumla ya Shilingi trilioni 1.36 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.65”. Ameeleza Kayombo.

Mkurugenzi huyo pia amewashukuru walipakodi wanaoendelea kulipa kodi zao kwa hiari na wakati huku akiwahimiza wale ambao bado wanasuasua kujitokeza kulipa kodi hizo na kuwataka wenye changamoto mbalimbali kufika katika ofisi za TRA. Kayombo amesema TRA bado inapokea maombi ya misamaha ya riba na adhabu katika malimbikizo ya madeni ya kodi za nyuma ambapo mpaka sasa, walipakodi takribani 1,950 wamewasilisha maombi ya misamaha ambayo yanafikia jumla ya Sh. 185.4 bilioni.

“Mwitikio wa walipakodi kuomba msamaha wa riba na adhabu ni mkubwa na unaridhisha na kuna baadhi ya walipakodi waliowasilisha maombi ambao wameshapewa majibu na wengine wako katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa maombi yao. Hivyo nachukua fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara ambao hawajawasilisha maombi wawahi kuwasilisha maombi hayo kabla ya tarehe 30 Novemba 2018”. Amesema Kayombo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter