Home FEDHAMIKOPO Bilioni 88 kusomesha maelfu elimu ya juu

Bilioni 88 kusomesha maelfu elimu ya juu

0 comment 208 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa, bodi hiyo imetangaza awamu ya kwanza ya walionufaika na mikopo yenye thamani ya Sh.88.36 bilioni kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kwa waombaji 25,532 ambapo kati ya wanafunzi hao, wanawake ni 9,447 huku wanaume wakiwa 16.805. Katika awamu hii ya kwanza, pia imeelezwa kuwa HESLB imetoa mikopo kwa wanafunzi wapatao 69 wanaosoma nje ya nchi kwa makubaliano maalum na nchi rafiki ambapo mikopo hiyo imegharimu takribani Sh. 850.35 milioni.

Katika maelezo yako Badru amesema kuwa kwa mwaka wa masomo 2018/2019, bajeti ya fedha za mikopo ya elimu ya juu ni Sh. 427.5 bilioni na kati ya fedha hizo, serikali tayari imetoa Sh. 137.06 bilioni zinazohitajika wakati vyuo vinafunguliwa mwishoni mwa mwezi Oktoba na Novemba mwanzoni kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi wapya na wale wanaoendelea na masomo.

Kuhusu upangaji mikopo kwa wanafunzi kwa wanafunzi wa mwaka wa pili na zaidi, Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo wa bodi hiyo Dk. Veronica Nyahende amesema kuwa wanafunzi hao wataendelea kupatiwa mikopo endapo wamefaulu na matokeo yao yamewasilishwa bodi pamoja an vyuo husika.

“Tunatoa mikopo ili mwanafunzi asome, kwa hiyo tutaendelea kuwapa mikopo wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo ikiwa tumepokea uthibitisho kuwa ana sifa za kuendelea na masomo katika mwaka unaoanza hivi punde”. Amesema Dk. Nyahende.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter