Home KILIMO Wizara ya Kilimo yaanza kukagua korosho

Wizara ya Kilimo yaanza kukagua korosho

0 comment 217 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga pamoja na viongozi wakuu wa wizara hiyo wameanza ziara ya katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ili kuhakiki korosho zilizopo katika maghala makuu, ikiwa ni siku moja tu baada ya Waziri Hasunga kuapishwa kuongoza wizara hiyo, hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.

Katika ziara hiyo, Waziri Hasunga atatembelea mkoa wa Mtwara akiongozana na Naibu wake Innocent Lugha Bashungwa na Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe watakaotembelea mkoa wa Lindi huku Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Siza Tumbo akitembelea mkoa wa Ruvuma.

Wakiwa katika ziara hiyo, viongozi hao wanatarajia kuhakiki usimamizi wa maghala ambao kwa sasa upo chini ya Bodi ya usimamizi wa stakabadhi ya ghala. Pamoja na hayo, watahakiki taarifa za uwa maghala kama zilivyopitishwa na bodi hiyo. Vilevile, viongozi hao watahakiki kiasi cha korosho kwa kupitia nyaraka za mapokezi ya zao hilo kwenye ghala ambazo zinawasilishwa na Vyama vya msingi (AMCOS) na baaadae kuoanisha taarifa hizo na taarifa zilizomo katika taarifa za stakabadhi ya ghala (Warehouse Report).

Ziara hiyo inawaleta pamoja viongozi kutoka Wizara ya kilimo, Ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya, Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI)-Naliendele, na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (WRRB).

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter