Home Uncategorized Vodacom Foundation yatoa elimu ya afya kwa vijana

Vodacom Foundation yatoa elimu ya afya kwa vijana

0 comment 237 views

Vodacom Foundation kushirikiana na PSI, wamafanya tamasha liitwalo ‘Kuwa Mjanja’ lililolenga vijana kupata elimu ya Afya.

Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald (katikati ) akiwa pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam, wakielekezwa na mtaalam wa ubunifu wa kazi za mikono Flora Richard jinsi ya kutengeneza bangiri za batiki wakati wa Tamasha la Kuwa Mjanja ambalo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya Afya iliyoandaliwa na PSI kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation.

Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald (watatu kushoto) akionyeshwa na Meneja miradi wa PSI Tanzania, Dkt. Anna Temba (wa pili kulia) ujumbe maalumu kwenye Tablet ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia elimu ya Afya kwa vijana wakati wa tamasha la Kuwa Mjanja lililofanyika katika shule ya Sekondari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya Afya lililoandaliwa na PSI kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation. Kutoka kushoto ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Goba Magreth Richard, Agnes John, Mhamasishaji wa Vijana PSI Semeni Likulo na Pendo Raphael (kulia)

Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam, wakijifunza elimu ya ujasiriamali wa kazi za mikono pamoja na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( Kulia) wakati wa tamasha la Kuwa Mjanja ambalo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya Afya, elimu ya ujasiriamali iliyoandaliwa na PSI kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation. Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya shule ya msingi Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter