Home FEDHA Mapato ya serikali yazidi kuongezeka Mirerani

Mapato ya serikali yazidi kuongezeka Mirerani

0 comment 106 views

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema mapato ya serikali yanayotokana na migodi ya Tanzanite Mirerani mkoani humo yameongezeka kutoka Sh. 402 milioni miezi kumi iliyopita hadi Sh. 2.1 bilioni kufuatia kujengwa kwa ukuta kuzunguka eneo hilo ili kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo. Mnyeti amesema hayo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya mkoa huo kwa Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye yupo wilayani Simanjaro kwa ziara ya kikazi.

“Ukuta unaendelea kuleta miujiza ya aina yake, serikali imefanya kazi kubwa kwa kukusanya Sh. 2.1 bilioni, ikiwa ni sawa na ongezeko la Sh. 1.7 bilioni sawa na asilimia 425. Kabla ya kujengwa ukuta kituo cha TRA Mirerani kilikuwa kikikusanya Sh. 402 milioni tu, lakini baada ya ukuta, kituo kimekusanya Sh. 2.1 bilioni ikiwa ni ongezeko la Sh. 1.7 bilioni. Sasa hii ndiyo miujiza ambayo mnapaswa kuijua, tumeongeza mapato kwa asilimia 425 hii ni ajabu, lakini ndio ukweli, hapo bado mrahaba”. Ameeleza Mnyeti.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kufuatia makusanyo kuongezeka, jamii imeendelea kupata imani na serikali kwani matokeo ya ujenzi wa ukuta huo yameanza kuonekana. kwa upande wake, Makamu wa Rais amepongeza jitihada kubwa zinazofanyika mkoani humo ili kuhakikisha pato la madini linaongezeka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter