Home KILIMO Watendaji waagizwa kusimamia ubora wa korosho

Watendaji waagizwa kusimamia ubora wa korosho

0 comment 67 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amewaagiza watendaji kutoka Bodi ya Korosho pamoja na wanaoendesha maghala kusimamia ubora wa korosho ili fedha za serikali zinazotolewa maalum kwa ajili ya ununuzi wa korosho za wakulima mikoani Lindi, Mtwara na Ruvuma zitumike ipasavyo. Waziri Hasunga amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara.

Hasunga ameeleza kuwa, kufuatia taarifa kuwa serikali kuanza kuwalipa wakulima wa zao hilo kusambaa katika maeneo mbalimbali, yamejitokeza matukio ya uwepo wa korosho chafu zilizotunzwa kwenye maghala tangu msimu wa 2016/2017 zikiwa hazina ubora unaotakiwa wa daraja la kwanza ili hali korosho za madaraja mengine hazijaanza kununuliwa.

“Nadhani wanafanya hivi ili wafaidike na hela za serikali, jambo hili hatuwezi kukubaliana nalo kwani tayari tumeshakamata tani 20 za korosho chafu kutoka kwenye ghala la Olam za Chama cha Ushirika cha Mnyawi Amcos kilichopo Nanyamba pamoja na Mbembaleo Amcos ambapo gunia tano za korosho chafu zimepatikana”. Amesema Waziri huyo.

Akizungumzia kuhusu kuanza malipo kwa wakulima wa korosho, Hasunga amesema mpaka sasa, vyama 35 tayari vimehakikiwa na serikali imeanza kulipa fedha zinazostahili.

“Vyama vilivyohakikiwa ni 35 lakini mpaka sasa kati ya hivyo vyama 6 vimeshaingiziwa fedha ambavyo ni Mtama Amsos, Kitomiki Amcos, Mnazimoja Amcos, Mtetesi Amcos, Chamana Amcos na Msafichema Amcos”. Amesema Waziri huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter