Home VIWANDAMIUNDOMBINU Wanaochimba visima bila kufuata sheria kubanwa

Wanaochimba visima bila kufuata sheria kubanwa

0 comment 111 views

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa ameitaka Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu kusimamia Sheria kwa kuwachukulia hatua wale wanaochimba visima bila kufuata taratibu zilizopo kwa mujibu wa Sheria ili kunusuru vyanzo vya maji. Waziri Mbarawa amesema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya upandaji miti katika vyanzi vya maji na kuongeza kuwa, Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) inayo maji yenye viwango vya ubora vya kimataifa hivyo hakuna sababu ya watu kuendelea kuchimba visima.

Kauli hiyo ya Waziri Mbarawa inakuja siku chache baada ya Bodi hiyo kutangaza kuanza operesheni ya kuwatafuta wote waliochimba visima vya maji na kutumia maji hayo pasipo kulipia kodi.

“Kuna Sheria ipo kabla ya kuchimba kisima unatakiwa kufanya, kuna utaratibu wa kufuata, unaenda kwa watu wa bonde unasema unataka kuchimba kisima wanakupa kibali cha kuchimba na baada ya hapo wanakuja kupima maji yanayotoka pale kuangalia ubora”. Amefafanua Prof, Mbarawa.

Kwa upande wake, Ofisa wa Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani amesema kufuatia agizo hilo, watahakikisha  wanasimamia Sheria ili kulibda vyanzo vya maji.

“Ni kweli kabisa hiki chanzo ni kikubwa kwa Dawasa kusambaza maji, namhakikishia Waziri kuwa tutafanya kazi ya kutunza vyanzo vya maji na kwa hapa tutaongeza kasi kwa kuanza kusimamia Sheria ya mita 60 kukaa mbali na vyanzo vya maji”. Ameeleza Ofisa huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter