Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mradi wa daraja Ziwa Victoria kuanza mwakani

Mradi wa daraja Ziwa Victoria kuanza mwakani

0 comment 102 views

Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa ametoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Mwanza na Geita kuchangamkia fursa za kiuchumi na kijamii zitakazojitokeza kufuatia ujenzi wa daraja litakalounganisha eneo la Kigongo na Busisi mkoani Mwanza. Naibu Waziri Kwandikwa ameeleza kuwa maandalizi ya ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3.2 yapo katika hatua ya usanifu wa kina na ujenzi wa mradi huo utaanza mara baada ya mkandarasi wake kutangazwa.

“Hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kazi ya ujenzi iwe nyepesi na wale watakaopata fursa za ajira fanyeni kazi kwa weledi, bidii na nidhamu”. Amesema Kwandikwa.

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa, serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya muda mrefu hivyo ni jukumu la wananchi kujiandaa na kubaini fursa za kiuchumi na kijamii na kuzitumia kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya amesema daraja hilo litakuwa na njia nne za kupitisha magari, njia ya watembea kwa miguu na vilevile litakuwa na kina kitakachoruhusu meli kupita chini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter