Home KILIMO Serikali yaongeza wataalamu wa kuhakiki korosho

Serikali yaongeza wataalamu wa kuhakiki korosho

0 comment 96 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amewaambia waandishi wa habari kuwa, timu ya wataalamu wa uhakiki wa wakulima wa korosho imeongezeka kutoka 11 hadi 20 katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ili kuharakisha uhakiki kwa ajili ya malipo ya wakulima. Waziri Hasunga amesema hayo mkoani Mtwara alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu hali ya ununuzi wa korosho.

Waziri huyo ameeleza kuwa wataalamu hao tayari wamewasili mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza uhakiki wa wakulima wa korosho ambapo mkoa huo utakuwa mkoa wa nne kuhakikiwa ukiungana na mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Aidha, Waziri Hasunga amesema hadi kufikia Desemba 01 2018, jumla ya vyama vya ushirika 212 kati ya vyama 504 katika mikoa hiyo mitatu ya kusini tayari vimeshahakikiwa wakati vyama 157 kati ya 617 vikiwa vimeshalipwa fedha zao. Hadi sasa, tayari Sh. 35,540,709,854 bilioni zimeshalipwa kwa wakulima wa korosho ambapo Kilo 10,769 milioni za korosho zimeshalipiwa. Katika mkoa wa Lindi, tayari Sh. 12.7 bilioni zimelipwa, mkoani Ruvuma ni Sh. 4.9 bilioni huku wakulima kutoka mkoa wa Mtwara wakilipwa Sh. 17.9 bilioni.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter