Home BIASHARAUWEKEZAJI Wizara ya Utalii yakaribisha wawekezaji

Wizara ya Utalii yakaribisha wawekezaji

0 comment 222 views

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu amesema Wizara hiyo imejipanga kikamilifu kuwasaidia wawekezaji walio na nia ya kuwekeza kwenye fukwe kwa ajili ya utalii. Kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mwaka jana ambapo aliagiza Wizara hiyo kuanzisha Kurugenzi ya fukwe itakayobeba jukumu la kusimamia na kuendeleza fukwe zote nchini, Wizara hiyo imeanza kuyatambua na kuainisha maeneo kwa ajili ya utalii wa fukwe katika kisiwa cha Mafia.

Katika maelezo yake, imeelezwa kuwa, lengo la serikali kuanzisha mkakati huo ni kuhakikisha mapato yanayotokana na sekta ya utalii kupitia utalii wa fukwe yanaongezeka na hivyo kukuza pato la taifa zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaib Nnunduma amesema kuwa wilaya yake inawakaribisha wawekezaji wenye malengo ya kuwekeza mahali hapo huku akiahidi kuwa, atatoa ushirikiano wa kutosha. Nnunduma amesema kuwa wilaya hiyo tayari imeshatenga maeneo maalum ya wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa hoteli za kiutalii katika maeneo ya ufukweni.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter