Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wajasiriamali wahimizwa kuchangamkia vitambulisho

Wajasiriamali wahimizwa kuchangamkia vitambulisho

0 comment 110 views

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, ameagiza wakuu wa wilaya mkoani humo kuhakikisha wanagawa vitambulisho vilivyotolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya wajasiriamali huku wakiwahamasisha wananchi wengi zaidi kujitokeza na kuvichukua kwani kutofanya hivyo ni uvunjifu wa Sheria. Mwanri amesema hayo wakati akigawa vitambulisho hivyo kwa wakuu wa wilaya na kuwataka wakuu hao kuwasaka wale wote ambao bado hawana vitambulisho hivyo.

“Wapo watu watakaokwambia sina kazi, kataa mwambie hapa kazi tu, huna kazi kosa la pili, la kwanza nimekukuta huna kitambulisho, la pili umesema huna kazi, unaishije, unakula wapi unalala wapi hapa mjini, tunataka uchukue kitambulisho, ili uende ukabangaize kwa ajili ya kutafuta chakula kwa watoto wako, uweze kupata nguo kwa ajili ya watoto wako”, ameeleza Mwanri na kuongeza:

“Kwa hiyo tukimkuta mtu hapa mjini hana kitambulisho ni kielelezo kwamba hana shughuli yoyote ni kosa lingine, unambana, unamkuta hashughuliki lakini kavaa vizuri, tunamuuliza unapata wapi mapato yako, tunajua huyu anaweza akawa muhujumu uchumi, au anapita nyumba za watu. Huna kitambulisho, hufanyi kazi, unaishi vizuri ni kosa lingine, unabambika makosa mpaka, wewe unaishi hapa mjini mtaa mmoja hadi mwingine unadoea, kosa lingine, makosa karibu matano hapo”. Amesema Mkuu huyo wa mkoa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter