Home BIASHARAUWEKEZAJI Hong Kong kuwekeza nchini

Hong Kong kuwekeza nchini

0 comment 94 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki amesema Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepata ujumbe kutoka kwa wafanyabiashara wa Hong Kong ambao wameonyesha dhamira ya kuwekeza katika viwanda, utalii pamoja na sekta ya afya hususani dawa. Waziri Kairuki ameeleza hayo baada ya kufanya kikao na wawekezaji na kusema kuwa, ujumbe uliowafikia umejikita zaidi katika kufanya utafiti katika uwekezaji.

“Ujumbe huu umekuwa ukifanya mazungumzo na Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD) na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na leo (jana) watatembelea eneo la uwekezaji wa Muhimbili lenye ukubwa wa heka 150 na la MSD huko Kibaha ili kuangalia fursa za uwekezaji katika ekta hiyo ya afya”. Amesema Waziri Kairuki.

Kwa upande wake, Mkuu wa msafara huo kwa niaba ya Balozi Mdogo wa Hong Kong Tanzania, Jessica So amesema fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini zimewavutia.

“Nchi ya Tanzania ina fursa mbalimbali za uwekezaji kwenye sekta mbalimbali, tumeamua kuwekeza kwenye sekta ya utalii, sekta ya dawa na sekta ya kilimo kwa kuongeza thamani mazao”. Amesema So.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe, amesema wameshafanya mazungumzo na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Hongkong ambayo inasimamia biashara na uwekezaji, ili kuhakikisha wafanyabiashara wengi zaidi wanajitokeza na kutumia fursa zilizopo Hongkong na Tanzania.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter