Home BENKI NMB yarudisha kwa jamii Mara

NMB yarudisha kwa jamii Mara

0 comment 100 views

Wananchi wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara wamepokea msaada wenye thamani ya Sh. 35 milioni kutoka benki ya NMB. Msaada huo uliojumuisha mabati 620, mbao 1,025, kilo 210 za misumari, vitanda 5 vya kawaida vya hospitali na mashuka 47 umeelekezwa kwenye sekta ya afya na elimu ambapo umesaidia hospitali ya Manyamanyama na shule tano za Nyasura, Nyamuswa, Mahanga, Nyabuzume, na Nyansirori.

Meneja wa benki hiyo kanda ya ziwa, Abraham Augustino amesema hadi sasa wametumia Milioni 110 kwa ajili ya kusaidia masuala ya kimaendeleo katika kanda hiyo na kueleza kuwa, wataendelea kutoa ushirikiano kwa serikali katika kuendeleza jamii.

Kamishna wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili ametoa shukurani zake za kwa NMB kwa msaada huo hasa katika kipindi hiki ambacho sekta ya elimu inahitaji mazingira rafiki yanayoweza kuwasaidia wanafunzi hasa wale waliomaliza elimu ya msingi na kuanza elimu ya sekondari.

Aidha, Kamishna huyo amewataka NMB kuhakikisha huduma zao za kifedha zinapatikana ipasavyo hasa kipindi hiki ambacho wakulima wa pamba wanavuna zao lao na kufanya malipo kwa njia ya benki kama serikali inavyoelekeza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter