Home FEDHA Makusanyo finyu yamkera Samia

Makusanyo finyu yamkera Samia

0 comment 92 views

Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji mkoani Singida kuhakikisha wanajiimarisha katika ukusanyaji mapato ya ndani katika halmashauri zao husika ili kuleta maendeleo kwa wananchi. Makamu wa Rais amesema hayo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji ya mkoa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, ambayo imeonyesha wastani wa makusanyo ya mapato kwa mkoa huo kwa sasa kuwa ni asilimia 39 tu.

“Makusanyo ya mapato yenu ni aibu tupu. Wakati wenzenu wanakusanya zaidi ya asilimia 80 ninyi mnakusanya asilimia 39 tu. Mnasubiri wenzenu wakusanye ninyi mje mgawiwe,” amesema Samia na kuongeza:

“Huu ni unyonyaji. Tumieni vyanzo vyenu mbalimbali vya mapato ili kujiletea maendeleo yenu na ustawi wa wananchi wenu”

Mbali na hayo, Makamu huyo pia amesisitiza viongozi wa ngazi mbalimbali mkoani humo kuondoa tofauti zao za kiutendaji na kuonya kuwa hali hiyo haitavumiliwa.

“Taarifa za ulinzi na usalama za mkoa zinaonyesha mahusiano baina ya baadhi ya viongozi na watendaji hapa kwenu zinaonesha hamko vizuri. Kila mmoja ana eneo lake la kazi, sasa mnachogombania ni nini”? Amehoji Samia.

Kwa upande wake, Dk. Nchimbi amekiri kuwa mkoa huo haufanyi vizuri katika makusanyo ya mapato na kusema hadi sasa, wamekusanya asilimia 39 tu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter