Home BENKI Benki ya Stanbic kuwashukuru wateja wao

Benki ya Stanbic kuwashukuru wateja wao

0 comment 130 views

Katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, wafanyakazi wa Benki ya Stanbic, matawi yote, imewapa wateja wake meseji za shukurani na zawadi mbalimbali kuwashukuru wateja wao kwa kuendelea kufanya miamala yao ya kibenki na benki hiyo.

Mteja wa Benki ya Stanbic, Aisha Sykes akimshukuru Bw. Fredrick Mushi, mhudumu wake wa benki, baada ya kumpatia ujumbe wa kumshukuru kwa kuwa mteja wa benki ya Stanbic. Benki ya Stanbic imesherehekea wiki hii ya huduma kwa wateja kwa kuwapa zawadi wateja wao na kuwashukuru kwa kuendelea kuwa wateja wa benki hiyo.

Mshauri wa wateja wa benki ya Stanbic akimpa mteja wake meseji ya shukurani kwa kufanya miamala yake ya kibenki na Stanbic wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Centre.

Meneja wa Benki ya Stanbic tawi la Centre, Bw. Adelhem Msiagi akimpa mteja wao ujumbe wa shukurani kwa kuchagua kufanya miamala yake ya kibenki na benki ya Stanbic wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Centre.

Mteja wa benki ya Stanbic, Ruth Bura akifurahia kupokea chupa ya kinywaji chake pendwa cha champagne kutoka kwa mhudumu wake wa benki, Edward Nyerere wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Centre.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter