Home FEDHA Barrick kuilipa serikali $300,000,000

Barrick kuilipa serikali $300,000,000

0 comment 105 views

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema serikali inategemea kupata Dola za Marekani 300,000,000 kutoka kampuni ya Barrick Gold mwezi machi mwaka huu. Waziri huyo amehakikisha kuwa nyaraka zote za makubaliano zimeshakamilika na kilichobaki ni utekelezaji tu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold kwa upande wa Afrika Mashariki ya Kati, Dk. Willem Jacobs amesema wamefanya mazungumzo na Rais John Magufuli ili kumhakikishia kuwa makubaliano yaliyofikiwa Oktoba mwaka juzi yanatekelezwa kufuatia kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Rand Gold ya Afrika Kusini kuungana na kampuni hiyo.

Pamoja na hayo, baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kuendeleza uwekezaji wa ubia baina ya serikali na kampuni ya Barrick na mgawanyo wa mapato ya kiuchumi kuwa asilimia 50 kwa 50.

Imeelezwa kuwa Dk. Jacobs amempongeza Rais Magufuli kwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi na kusema kuwa anaunga mkono jitihada hizo kwani ni muelekeo sahihi kwa nchi za Afrika.

“Mimi kama mwafrika na sisi wote kama waafrika. Anachokifanya Rais Magufuli ni sahihi kabisa, anahakikisha utajiri wa rasilimali unabainishwa na unawanufaisha watanzania ndiyo maana tupo hapa kwa sababu tunakubaliana na Rais”. Amesema Dk. Jacobs kwa mujibu wa taarifa hiyo.

 

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter