Home BENKI Huduma 70 Standard Chartered sasa kiganjani kwako

Huduma 70 Standard Chartered sasa kiganjani kwako

0 comment 134 views

Benki ya Standard Chartered imezindua huduma mpya inayowawezesha wateja wake kupata huduma hadi 70 kupitia simu za kisasa (smartphone) bila kufika katika tawi lolote la benki hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sanjay Rughani amesema wanategemea kupata wateja 40,000 hadi kufikia mwezi Desemba kutokana na kuanza kwa teknolojia hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es salaam hapo jana.

“Tanzania imekuwa nchi ya tatu kuzindua mfumo huu miongoni mwa nchi 70 ambazo Standard Chartered tunatoa huduma, mfumo huu unarahisisha huduma kwa kuwa na gharama ndogo lakini pia kwa kuwa matumizi ya simu ni makubwa utasaidia kujumuisha watanzania wengi katika huduma za kifedha”. Amesema Rughani.

Hata hivyo Mkuu wa benki hiyo ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati, Jaydeep Gupta ameeleza kuwa hadi sasa  wametumia takribani Dola za kimarekani Bilioni 1.5 kuendeleza teknolojia mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitatu katika benki hiyo na wanaendelea kufanya uzinduzi katika nchi nyingine ili wateja wao waweze kufurahia huduma.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter