Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Bilinith Mahenge amewataka wakulima kuacha kuishi kwa mazoea kwa kulima mazao ambayo hayawaletei faida na kuchangamkia fursa ya mazao yanayostawi zaidi mkoani humo kama mtama,uwele,mpunga,karanga,muhogo,alizeti, na zabibu ili kuongeza pato lao na la taifa.
Muheshimiwa huyo amesema katika mazao matano ya kimkakati kutokana na serikali mazao mawili yanastawi vizuri mkoani humo, mazao hayo ameyataja kuwa ni Pamba na Alizeti. Pia amewataka wakulima kupunguza kulima mazao yanayotaka mvua kubwa kama mahindi na kushughulika zaidi na mazao yanayoitaji mvua ya kawaida na yenye faida zaidi.
Dk.Mahenge ametaja Zabibu kuwa moja ya zao lenye soko kubwa mkoani humo na hivyo kuwataka wakulima wa zao hilo kulima kwa wingi ili waweze kufaidika zaidi na kuleta maendeleo nchini.
Aidha, Mkuu huyo amekua akipata ushirikiano kutoka kwa wakuu wa wilaya wa mkoani humo ili kuhakikisha kuwa kila mkulima anaweza kulima ekari mbili na kuendelea mazao ya chakula na biashara ili aweze kujipatia maendeleo ya kiuchumi na kifamilia.