Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mabadiliko kufanyika awamu ya pili mwendokasi

Mabadiliko kufanyika awamu ya pili mwendokasi

0 comment 115 views

Wakala wa mabasi yaendayo haraka ‘mwendokasi’ (DART) imeeleza kuwa inatarajia kupata mwekezaji wa kimataifa hadi kufikia Julai mwaka huu na kwamba, watatangaza zabuni hiyo ifikapo mwezi Machi. Kufuatia changamoto za uendeshaji zilizojitokeza awamu ya kwanza ya mradi, imeelezwa kuwa hakutakuwa na mwendeshaji wa mpito katika awamu ya pili inayotarajiwa kuanza mwezi ujao na kampuni itakayotoa huduma itapatikana wakati wa hatua za mwisho za kukamilika mradi.

Mtendaji Mkuu wa DART, Ronald Rwakatale, amesema kuwa hadi sasa mwendeshaji wa huduma za usafiri wa mpito UDART ana mabasi 140 ambayo hayatoshelezi wanaotumia usafiri huo na hivyo mwendeshaji mpya anategemea kutatua tatizo hilo kwa kuongeza mabasi ambayo yatafika 305 ili kumalizana na changamoto hiyo.

“Ni kweli kwa sasa tuna changamoto kubwa ya usafiri kwa kuwapo ongezeko kubwa la watu na mabasi kuwa machache ,huku mwendeshaji wa mpito akikabiliwa na changamoto mbalimbali, jambo ambalo tumejifunza katika awamu hii ya pili inayoanza kampuni ya kuendesha mradi itapatikana mapema na hakutakuwa na mwendeshaji wa mpito”. Amesema Rwakatale.

Aidha, amesisitiza makampuni ya kizalendo kuchangamkia fursa kama ukatishaji tiketi na fursa nyingine katika awamu hiyo ya pili ili waweze kunufaika kiuchumi. Pia Mtendaji huyo amesema kuwa awamu hiyo ya pili itahusisha ujenzi katika barabara za Kilwa, Kawawa, Sokoine, Gerezani, Bandarini na Chang’ombe ambayo itakuwa na urefu wa kilomita 20.3, ambapo ujenzi wa majengo, karakana na kituo kikuu utatumia miaka miwili huku ujenzi wa barabara ambayo itahusisha na barabara ya juu katika maeneo mawili yenyewe ikitumia miaka mitatu kukamilika.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter