Home BENKI Wafanyabiashara washauriwa kuchangamkia benki

Wafanyabiashara washauriwa kuchangamkia benki

0 comment 128 views

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira, amewasisitiza wadau wa sekta ya biashara kutumia fursa zinazotolewa na benki hapa nchini ili kukuza biashara zao. Mghwira amesema hayo wakati akifungua semina iliyoandaliwa na benki ya CRDB huko Moshi.

Mkuu huyo ameeleza kuwa lengo la CRDB kuandaa semina kama hizo ni wajasiliamali na wafanyabiashara kujipatia ujuzi na kuendeleza biashara zao kupitia mikopo nafuu, huku akieleza kuwa, ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuchangamkia fursa hizo. Mghwira amesema kuwa serikali inashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ikiwemo benki ya CRDB  ili kuhakikisha mazingira ya biashara ni ya kuridhisha.

Aidha, RC huyo ameongezea kuwa, suala la CRDB kuvumbua njia za kuweza kukuza na kupanua ujasiliamali inaonyesha jinsi gani benki hiyo inataka kuunga mkono mpango wa  serikali wa kujenga uchumi endelevu ambao utagusa kila maeneo ya kiuchumi.

“Serikali imeshatoa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo, benki inatakiwa iende zaidi kwa kuanzisha mikopo ya gharama nafuu kwa ajili yao, ili kupanua biashara zao”. Amesema Mkuu huyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nsekela, amewahakikishia wajasiriamali kuwa benki hiyo imejiandaa kikamilifu ili kuhakikisha wanapata huduma za kifedha kikamilifu.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter