Home FEDHA Bajeti ya serikali 2019/2020 hii hapa

Bajeti ya serikali 2019/2020 hii hapa

0 comment 113 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amewasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa jijini Dodoma ambapo bajeti ya serikali kwa mwaka 2019/2020 inatarajiwa kuwa Sh. 33.105 trilioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.9 ikilinganishwa na bajeti ya 2018/2019 ya Sh. 32.476 trilioni.

Dk. Mpango ameeleza kuwa, bajeti hiyo imeelekezwa hasa kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini hasa kilimo, madini na gesi asilia ili kutimiza Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Miradi hyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia, uanzishwaji na uendelezaji wa kanda maalumu za kiuchumi na kongane za viwanda, viwanda vyakuongeza thamani mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, kuongeza thamani ya madini na usimamizi endelevu wa rasilimali misitu”. Amesema Waziri Mpango.

Vilevile ametaja maeneo ambayo yatapewa kipaumbele kuwa ni pamoja na kutoa elimu ya msingi bila ada, kupunguza vifo vya wakina mama vinavyotokana na uzazi, kutekeleza programu ya sekta ya elimu, ujenzi na kukarabati vyuo vya ufundi vilivyopo nchini na kuboresha huduma ya maji hususani maeneo ya vijijini.

Waziri huyo ametaja maeneo mengine ambayo yatafanyiwa maboresho kuwa ni pamoja mazingira ya biashara, uwekezaji na miundombinu.

“Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa kufua umeme wa maji Rufiji (Megawati 2,115), kuboresha Shirika la Ndege la Tanzania, ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Standard Gauge na kuendelea na utekelezaji wa mpango wa kuboresha mfumo wa udhibiti wa biashara na uwekezaji”. Amesema Dk. Mpango.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter