Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wajasiriamali wahamasishwa ‘utatu wa biashara’

Wajasiriamali wahamasishwa ‘utatu wa biashara’

0 comment 115 views

Mwenyekiti wa taasisi ya Sirolli ya nchini Marekani, Dk. Ernest Sirolli amesema ili kupata maendeleo, kuna umuhimu mkubwa kwa wajasiliamali kufanya biashara zao kwa kuzingatia kanuni ya utatu. Dk. Sirolli amesema hayo kwa wajasiriamali wilayani Mbozi mkoani Songwe kwenye mradi wa uwekezaji wa biashara (Sirolli) na kufafanua kuwa, kanuni ya utatu ni timu ambayo inawahusisha wasimamizi wa uzalishaji, watafuta masoko na wasimamizi wa fedha ili kuhakikisha biashara inaenda vizuri, jambo ambalo wafanyabiashara wengi hawafanyi wakihofia malipo ya kuwalipa wataalamu hao hivyo kusababisha biashara zao kukosa mwenendo mzuri.

Pamoja na hayo, pia ameelezea kuwa mradi huo ulioanza mwaka 2017 unafadhiliwa na shirika la kimataifa la Heifer International na unatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu.

“Tunatoa ushauri bure na kwa usiri kwa mtu yeyote anaehitaji, mwenye wazo la biashara, ni muhimu mjasiliamali kujua soko lilipo, ubora wa bidhaa zinazohitajika na kuimalisha mifumo ya usimamizi wa fedha”. Amesema Dk. Sirolli.

Naye Makamu Mwenyekiti wa shirika la Heifer International, Rose Marando amesema kampuni hiyo imeona kuna umuhimu mkubwa wa kuwapa elimu na kutekeleza mradi huo kwa sababu wajasiliamali wengi wanapitia changamoto nyingi na kukata tamaa au kutumia fedha za biashara kwa mambo yao binafsi, jambo ambalo sio sawa.

“Mara nyingi tumeona mjasiliamali huyo anazalisha bidhaa, anatafuta masoko mwenyewe na anatunza fedha mwenyewe hali ambayo inafika wakati vyote vinakuwa vigumu kwake, sasa tumekuja na kitu kinaitwa ‘utatu wa biashara au business psychology (saikolojia ya biashara au Trinity of Management)”. Ameeleza Makamu huyo.

Aidha, Afisa Uhusiano wa shirika hilo, Mercy Nyanda amewasisitiza wajasiliamali kutumia fursa hiyo kujifunza na kuchukua hatua katika biashara na shughuli wanazofanya.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter