Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wajasiriamali wahimizwa ubora

Wajasiriamali wahimizwa ubora

0 comment 140 views

Mratibu wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata) Arusha, Richard Masandika ametoa wito kwa wajasiriamali kujikita zaidi katika utengenezaji wa bidhaa zenye viwango na ubora ambazo zitauzwa kwa bei nafuu ili kujihakikishia masoko ndani na nje ya nchi. Masandika ameshauri hayo wakati akifungua mafunzo ya usindikaji mazao ya vyakula na mifugo na kuwasisitiza wajasiriamali hao kutumia maarifa wanayopatiwa kupitia mafunzo hayo.

“Nawataka mtumie vizuri mafunzo haya mliyoyapata, msiishie njiani, tumieni weledi kutengeneza bidhaa bora zenye viwango ambazo zitapata masoko kwa urahisi ndani na nje ya nchi”. Amesema Mratibu huyo.

Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO) mkoani Arusha, Bahati Mkopi amewataka wajasiriamali wote wanaohitaji ujuzi zaidi kwenye masuala ya usindikaji kufika ofisi za shirika hilo ili kupatiwa mafunzo mbalimbali pamoja na elimu.

Pamoja na hayo, shirika hilo pia limeendelea kuwasisitiza wajasiriamali kuwa na vitambulisho vya wajasiriamali ambavyo vinatolewa nchini kote ili biashara na bidhaa zao zirasimishwe rasmi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter